Kremlin: Mazungumzo na Kiev yatafanyika vikwazo vikiondolewa
22 Aprili 2025Matangazo
Msemaji wa ikulu ya Urusi, Kremlin Dmitry Peskov, amesema ikiwa upande wa Ukraine uko wazi kwa mazungumzo, hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kuondoa vikwazo kwenye njia ya mawasiliano.
Maafisa wa US na Russia wakutana Saudi Arabia kujadili usitishaji vita Ukraine
Katika hatua nyingine, Urusi imeushambulia mji wa bandari wa Odesa nchini Ukraine kwa droni huku mabomu yakilenga Zaporizhia. Haya ni kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo katika wakati ambapo ikulu ya Kremlin imeonya tena kwamba wapatanishi huenda wakashindwa kupata ufanisi katika mazungumzo ya amani.
Wakati huo huo, maafisa wa Ukraine, Uingereza, Ufaransa na Marekani wanatarajiwa kukutana mjini London kesho Jumatano kwa mazungumzo kuhusu vita hivyo.