MigogoroKorea Kusini
Korea Kusini yaanza kuondoa vipaza sauti kwenye mpaka
4 Agosti 2025Matangazo
Vipaza sauti hivyo vilikuwa vikitumiwa kueneza propaganda dhidi ya Korea Kaskazini, lakini serikali mpya ya kiliberali ya Korea Kusini ilisitisha matangazo hayo mwezi Juni kama ishara ya maridhiano.
Serikali hiyo inaangazia kurejesha uaminifu na mazungumzo na Pyongyang ambayo imekata mahusiano na Korea Kusini kwa kiasi kikubwa katika siku za karibuni.
Korea Kaskazini ambayo inajilinda sana dhidi ya ukosoaji wa nje kuhusiana na utawala wake wa kiimla na kiongozi wake Kim Jong Un haikusema chochote kuhusiana na hatua hiyo.