SiasaAsia
Korea Kusini, Marekani zaanza luteka kubwa ya kijeshi
18 Agosti 2025Matangazo
Mazoezi hayo yanawahusisha wanajeshi 21,00 kutoka pande zote mbili. Korea Kusini na Marekani zimeanza kufanya mazoezi hayo ili kukabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini. Luteka hiyo ya kijeshi itawahusisha wanajeshi 21,00 kutoka pande zote mbili. Mazoezi mengine makubwa zaidi ya hayo yamepangwa kufanyika mwezi machi.
Korea Kaskazini kwa upande wake imeonya kuwa mazoezi ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini yatazidisha mivutano ya kikanda na imeapa kuchukua hatua kwa uchokozi wowote utakaofanywa dhidi yake.
Luteka hiyo ya kila mwaka ambayo hufanyika Korea Kusini inaendelea wakati Rais mpya wa Korea Kusini Lee Jae Myung akijiandaa kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump Agosti 25.