SiasaAsia
Korea Kaskazini yaahidi kuendelea kuiunga mkono Urusi
13 Julai 2025Matangazo
Kim Jong Un amesema nchi hizo mbili zina mitazamo inayofanana kuhusu masuala yote ya kimkakati na Pyongyang iko tayari kuunga mkono hatua zote za utawala wa Moscow katika kukabiliana na kiini cha mzozo wa Ukraine.
Wakati huohuo Waziri wa Mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amezionya Marekani, Korea Kusini na Japan dhidi ya kuunda ushirika wa kiusalama unaoilenga Korea Kaskazini.
Pyongyang imekuwa ikiiunga mkono Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine kwa kuipa silaha na wanajeshi. Nazo Marekani, Korea Kusini na Japan zimetanua luteka za pamoja za kijeshi kutokana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini unaozidi kukua.