MigogoroKorea Kaskazini
Korea Kaskazini yaanza kuchunguza ajali ya meli ya kivita
23 Mei 2025Matangazo
Korea Kaskazini ilisema jana kwamba "ajali mbaya ilitokea" katika hafla ya uzinduzi wa meli hiyo ya tani 5,000, baada ya sehemu ya chini ya meli kuvunjika, hatua iliyomghadhabisha kiongozi wake, Kim Jong Un aliyeiita ajali hiyo "kitendo cha kihalifu".
Shirika rasmi la Habari la Korea Kaskazini (KCNA), hata hivyo, limesema leo kwamba ukaguzi uliofanywa chini ya maji na ndani wa meli hiyo ulithibitisha kwamba, hakukuwa na matundu chini ya meli tofauti na ilivyoripotiwa awali.
Limesema, kiwango cha uharibifu "si kikubwa" ingawa liliongeza kuwa ilikuwa ni muhimu chanzo cha ajali hiyo kuweka wazi.