Kongo yatahadharisha kuhusu Kimeta kwa wanyama
11 Aprili 2025Shirika hilo la uhifadhi wa mazingira nchini Congo, ICCN limeeleza kuwa ugonjwa huo unaweza kuwa na athari kubwa sio tu kwa wanyama bali pia kwa jamii zinazotegemea rasilimali za mbuga hii. Katika tangazao lao la tarehe 8 Aprili, wataalamu wa afya na wa wanyama wamesema, viboko wasiopungua 50 wamekufa kutokana na virusi ambavyo vina sumu ya kimeta kwenye ziwa Eduard jambo ambalo ni tishio kubwa kwa viumbe hao.
Uchunguzi wathibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa kimeta
Methode Uhoze, afisa na msemaji wa taasisi hiyo ya uhifadhi wa mazingira mkoani kivu kaskazini, amesema kuanzia mwezi huu wa nne, waligundua kwamba kuna viboko vilivyo kufa na vingine vilionesha alama za ugonjwa, na baada yakutumwa kwa waataalamu wa afya kwenye eneo hilo walichukua sampuli nakuthibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo wa kimeta.
Picha zilizosambazwa na wakazi wanaoishi kando na ziwa Eduard ambalo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi mkoani kivu kaskazini, zilionesha miili ya viboko ikielea kwenye mto Ishasa katika wilaya ya Rustruru huku miili mingine ikiwa imekwama ndani ya tope Kando na ziwa hilo lililo tajiri kwa samaki.
Uhoze ameongeza kuwa sio mara ya kwanza kwa ugonjwa huu kutokea .
Vifo vya viboko ni hatari kwa binadamu
Akizungumza na DW, Josué KAMBASU mwanaharakati wa mazingira na afisa mkuu wa uvuvi kwenye ziwa hilo amesema kuendelea kufariki kwa viboki hivyo kutashababisa hatari kubwa kwasababu wananchi wanakunywa maji ya bahari .
Katika hatua za kisheria, ICCN imeanzisha operesheni za kukusanya taarifa zaidi na kuihamasisha jamii kuhusu hatari zinazoweza kutokea. Aidha,Wananchi wanashauriwa kuwa makini na kuzingatia usafi wa mazingira ili kuzuia kuenea kwaugonjwa huo.
Wakazi washauriwa kuchukuwa tahadhari
Katika tangazo lililotolewa siku ya jumanne wiki hii, ICCN iliwataka wakazi kuwa mbali na wanyamapori na kuchemsha maji yanayotoka kwenye chemchem zinazotoka kwenye ziwa Eduard kabla ya kunywa.
Taarifa zinasema kuwa hifadhi ya Virunga inakadiriwa kuwa na viboko 1200 ambao wanashambuliwa kwa sasa na sumu hiyo iliyo ardhini na vyanzo vya ndani vimeeleza kwamba wakazi wa eneo hilo wanakabiliwa na kitisho kikubwa.