Utawala wa sheriaAfrika
Kongo yasitisha kwa muda uuzaji wa madini ya Kobalti
10 Machi 2025Matangazo
Serikali ya Kongo imesema hatua hiyo itadumu kwa kwa kipindi cha miezi minne ambapo hakutakuwa na mauzo ya madini hayo muhimu yanayotumika kutengeneza betri za magari. Imesema hatua hiyo inalenga kuleta utulivu katika soko.
Kwa mujibu wa Utafiti wa Jiolojia wa Marekani wa mwaka 2024, Kongo ilizalisha asilimia 76 ya Kobalti duniani, lakini katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita bei ya madini hayo imeshuka kwa asilimia 75 hicho kikiwa ni kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha miaka minane.
Soma pia:M23 wachukua udhibiti wa maeneo ya uchimbaji madini Kongo
Hata hivyo wataalamu wametahadharisha kwamba marufuku hiyo itakuwa na athati mbaya katika uchumi wa Kongo.