Kongo yashawishi mauaji ya halaiki yatambuliwe mashariki
10 Septemba 2025Matangazo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imezindua kampeni katika Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne ikitaka kutambuliwa kimataifa kwa "mauaji ya halaiki" dhidi ya watu wa mashariki mwa Kongo.
Waziri anayeshughulikia masuala ya haki za binadamu wa Kongo Samuel Mbemba aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Ulaya huko Geneva kwamba wanafanya kampeni ili dunia ivunje ukimya wake" kwa kuwa hakuna mtu anayethubutu kutamka neno mauaji ya halaiki.
Mbemba amesema wameanzia Geneva, watakwenda New York" kuwatanabahisha viongozi watambue kwamba kinachotokea nchini Kongo kinastahili kutajwa" kama mauaji ya halaiki.