MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Kongo yakanusha taarifa za kukamatwa wapiganaji 20
3 Machi 2025Matangazo
Taarifa ya jeshi hilo imetolewa baada ya kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda mashariki mwa Kongo, kutangaza kuwa limewakamata wapiganaji wa kundi la FDLR, lililoundwa na jamii ya Wahutu inaoaminika walitekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Jeshi la Kongo limesema madai hayo ya M23 siyo ya kweli na hata mkanda wa video ulioonesha wapiganaji waliokamatwa Kongo wakikabidhiwa kwa Rwanda ni wa "kughushi".
Kwa muda mrefu Rwanda imekuwa ikidai uwepo wa kundi la FDLR mashariki mwa Kongo na kutumia madai hayo kuhalalisha uungaji wake mkono kwa kundi la M23.