Kongo na Rwanda kutia saini makubaliano ya kumaliza vita
27 Juni 2025Makubaliano hayo pia yataiwezesha serikali ya Marekani kufikia madini muhimu katika eneo hilo linalokumbwa ambalo ni tajiri pia kwa madini.
Vipengee muhimu kwenye makubaliano hayo ni pamoja na kuheshimu mipaka, kujiepusha na uhasama na kuyapokonya silaha makundi yote yasiyo ya kiserikali.
Hata hivyo mashirika ya kiraia ya Kongo yameelezea wasiwsai wao kuhusu makubalano hayo yanayodai hayakuzingatia sababu za msingi za machafuko.
Rwanda na DRC waafikiana makubaliano ya awali ya amani
Kongo imekuwa ikikabiliwa na migogoro kwa muda mrefu huku kukiwa na makundi yaliyojihami zaidi ya 100 ya waasi. Kundi lililo na umaarufu zaidi ni lile la waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, ambapo hatua ya kutanua uwezo wao Mashariki mwa DRC imesababisha mauaji ya maelfu ya watu.
Machafuko yamesababisha watu takriban milioni nane kupoteza makazi yao na Umoja wa Mataifa umeielezea hali hiyo, kama moja ya migogoro mikubwa ya kibinaadamu kushuhudiwa duniani.