Kongo na M23 watangaza kusitisha mapigano
24 Aprili 2025Matangazo
Wameyasema haya wakati wakifanya juhudi za usitishwaji wa kudumu wa mapigano.
Tangazo hilo lililotolewa na msemaji wa M23 katika televisheni ya taifa nchini Kongo, linafuatia mazungumzo yaliyofanyika chini ya upatanishi wa Qatar.
Pande hizo mbili zimesema zimekubaliana kuendelea na juhudi za kuukamilisha mchakato wa usitishwaji mapigano katika mzozo huo ulioshuhudia M23 kuiteka miji kadhaa muhimu katika eneo la mashariki mwa Kongo lililozongwa na mapigano.
Tangu mwaka 2021, makubaliano sita ya kusitisha mapigano yamefikiwa ila yakavunjika.