Kongo: MSF yaonya kuongezeka ghasia eneo la Walikale
3 Aprili 2025Shirika hilo limesema, shughuli zake zimeathirika pakubwa kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 wanaosaidiwa na jeshi la Rwanda.
Katika tangazo lake, shirika hilo lisilo la kiserikali la madaktari wasio na mipaka, MSF limetoa tahadhadhari kuhusiana na hatari inayotokana na uhaba wa dawa muhimu katika hospitali kuu ya Walikale, ikiwa mapigano yataendelea katika eneo hilo.
Tangu kuanza kwa mapigano kati ya kundi la wapiganaji wa M23/AFC na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na vijana wazalendo, karibu asilimia 80 ya watu wameuhama mji huo huku wengine zaidi ya 700 wakiwa wamepatiwa hifadhi kwenye hospitali kuu ya Walikale ambayo inakabiliwa na uhaba wa vifaa muhimu kwa ajili ya wagonjwa. Imen Ben Othmen, Mratibu wa MSF wilayani Walikale ameripoti juu ya kusikika kwa milio ya silaha nzito.
Soma pia:Je, uhalifu mashariki mwa Kongo ni "mauaji ya kimbari" ?
"kwakusikia milio ya silaha nzito wakazi zaidi ya 700 wamekimbilia katika hspitali hii ya walikali jambo ambalo linasababisha uhataji mwingi wa vifaa na hata dawa kwa ajili ya wagonjwa .wiki mbili zili pita mabomu yalilenga hospitali nakuathiri vibaya majengo yetu pia baadhi ya magari yaliharibiwa ".
Shirika hilo hata hivyo, limetoa wito wa kuimarishwa kwa usalama ili kuwezesha utoaji wa huduma za Afya kwa wanaohitaji, huku likihamasisha jamii na wadau wa kimataifa kuchukua hatua za haraka, ameeleza Ben Othmen kwenye ripoti hiyo.
Kuathirika kwa miundombinu ya afya
Majengo yanayotoa huduma za Afya katika eneo hilo lenye uajiri yameathirika pakubwa kutokana na vita hivyo vinavyoendelea kusambaa na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi wanao hitaji huduma za msingi, imeelezea ripoti hiyo.
Mamlaka Gueli mwanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu mashariki mwa Kongo, amesema mashambulizi ya pande zote yameendelea kutatiza usalama katika eneo hilo.
"tatizo kubwa lililopo ni kwamba uongozi wa hao wazalendo haueleweki kabisa, mapigano kati ya pande zote mbili yanawakoseha amani wananchi na kuongeza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Kwetu kama raia tunachohitaji ni usitishwaji wa vita kati ya FARDC na M23".
Soma pia:Baraza la Usalama la UN kuchukuwa hatua kali dhidi ya Kongo
Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF pamoja na mashirika mengine ya kiutu yamekumbwa na changamoto kubwa ikiwa ni pamoja nakushindwa kuwafikishia misaada maelfu ya raia wanaohangika kutokana na vita katika wilaya ya Walikale iliyo umabli wa kilomita 235 kutoka Goma.