Kongamano la Vyombo vya Habari (GMF) laanza mjini Bonn
7 Julai 2025Matangazo
Wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka pande zote za dunia watajadiliana kuhusu mikakati ya kuleta mshikamano katika kipindi hiki kilichogubikwa na migawanyiko duniani na katika wakati ambapo dunia inakabiliwa na tawala za kimabavu na kubinywa kwa uhuru wa habari.
GMF: Kuchangiana Masuluhisho dunia inapokabiliwa na migogo
Shirika la habari la kimataifa la DW linakusudia kukabiliana na hali hiyo kupitia jukwaa hili la habari la siku mbili linaloanza hii leo na kumalizika hapo kesho Jumanne
Kauli mbiu ya Kongamano la mwaka huu ni "Kuvunja vizuizi na kujenga madaraja."