Kongamano la kimataifa la ufadhili lafungua pazia Uhispania
30 Juni 2025Matangazo
Viongozi wa dunia wakiwemo marais na mawaziri wakuu 70, wanasaka njia za kukabiliana na pengo linalozidi kuongezeka baina ya nchi tajiri na masikini na wanatarajia kukusanya trilioni za dola zinazopaswa kutumika kuliziba pengo hilo kufikia mwaka 2030.
Marekani chini ya utawala wa rais Donald Trump, ambayo ilikuwa mfadhili mkuu, imesusia kongamano hilo la siku nne linalofanyika wakati mataifa mengi yakiwa yamelemewa na mizigo ya madeni, kuporomoka kwa uwekezaji, kupunguwa kwa misaada ya kimataifa na kuongezeka kwa vikwazo vya kibiashara.