Kompany: Bayern haitabadilisha malengo licha ya majeruhi
8 Aprili 2025Matangazo
Akizungumza kabla ya mechi hiyo ya mkondo wa kwanza, Kompany amesema wachezaji watakaopata nafasi ya kucheza leo watahakikisha wanapata matokeo mazuri.
Bayern huenda wasiwe na kiungo Jamal Musiala, beki wa kupanda na kushuka Alphonso Davis na mabeki Dayot Upamecano na Hiroki Ito kwa wiki kadhaa. Nahodha na kipa Manuel Neuer, winga Kingsley Coman na kiungo Aleksandar Pavlovic watakosa mechi ya Jumanne na huenda wakakosa mechi ya marudiano.
Mechi ya Jumanne ni marudio ya fainali ya 2010 ambapo Bayern ilipoteza 2 - 0 dhidi ya Inter iliyokuwa ikifundishwa na Jose Mourinho. Fainali ya mwaka huu itachezwa katika dimba la Bayern - Allianz Arena, mjini Munich. Katika mechi nyingine ya leo, Arsenal watawakaribisha mabingwa watetezi Real Madrid.