KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA NA LA UJERUMANI:
22 Agosti 2005KOMBE LA DFB :
Mabingwa wa Kombe la shirikisho la kabumbu la Ujerumani msimu uliopita Bayern Munich, walianza vyema kutetea taji lao walipowazaba MSV Neuruppin timu ya daraja ya 4 mabao 4:0.
Mlinzi wa Ufaransa Valerie Ismael alitia bao lake la kwanza kwa Bayern Munich tangu kujiunga na klabu hiyo msimu huu kutoka Werder Bremen.Kocha Felix Magath aliamua kuwapumzisha staid Michael ballack na Roy Makaay nah ii iliwafanya mabingwa wasiwe hatari sana katika lango la chjipukizi hao wa daraja ya 4.Hatahivyo, mabao 4:0 yalitosha.
Stutgart ilitokwa na jasho kabla jana kuchechemea kuingia duru ya pili ya kombe hili.Stuttgart ilibidi kurefusha mchezo ndipo iondoke na ushindi dhidi ya timu ya kijijini ya Hoffenheim kwa mabao 4-3.Stuttgart imevuna hadi sasa pointi 1 tu tangu kuanza Bundesliga-Ligi ya Ujerumani wiki 2 nyuma.
Klabu zote nyengine za daraja ya kwanza zimevuka salama duru hii isipokua FC Cologne iliolazwa mabao 2:1 na Kickers Offenbach hapo jumamosi.Borussia Dortmund inakamilisha duru hii ya kwanza ya Kombe hili leo jioni itakapokutana na Eintracht Braunschweig.
Katika Ligi ya Uingereza-Premier League-Chelsea, iliitimua jana Arsenal kwa bao 1:0-bao alilotia Muivory Coast Didier Drogba na sio Mghana Michael Essien aliejiunga hivi majuzi tu na Chelsea.Drogba aliufumania mlango wa Arsenal mnamo dakika ya 73 ya mchezo.Huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Chelsea dhidi ya Arsenal katika Ligi ya Uingereza tangu kupita miaka 10.
Stadi wa Brazil-Robinho alishangiria jana mabao yake 2 ya mwisho kwa klabu yake anayoiaga ya Santos kwa mabao 2 ya mikwaju ya penalty.Santos iliirarua Figueirense jana kwa mabao 4-3.
Chipukizi kadhaa walifika uwanjani kumuaga Robinho na wachezaji wenzake wakamnyanyua na kumbeba kitikiti nae baadae akipiga magoti na kuubusu uwanja.
Robinho anajiunga na Real Madrid ya Spain.
Mabingwa watetezi wa Afrika Enyimba ya Nigeria, waliitoa jana Ajax Cape Town ya Afrika Kusini kwa mabao 2-0 katika changamoto za Kombe la klabu bingwa barani Africa.Hivyo Enyimba iko njiani kukata tiketi yake ya nusu-finali ya kombe hili na kukata mwishoe kiu chake cha kulitwa Kombe mara tatu mfululizo.
Ushindi wa nyumbani umeiimarisha Enyimba kuwa nafasi ya pili nyuma ya Al Ahly ya Misri imnayoongoza .Al Ahly imezkma raja Casablanca ya Morocco na kuondoka nayo suluhu bao 1-1.
Dakika 3 kabla ya firimbi ya mwisho kulia ilitia mabao 2 na kuipiga kumbo Ajax.
Bingwa mara mbili wa olimpik msichana wa Uingereza Kelly Holmes alimudu tu kuimaliza mkiani mwa mbio za mita 800 wakati wa mashindano ya Grand Prix ya Uingereza jana.
Holmes alishinda medali za dhahabu za Olimpik mwaka jana mjini Athens alipom piku maria Mutola wa Msumbiji katika mita 800 na medali nyengine katika mita 1500.
Kelly mwenye umri wa miaka 35 na aliekua ameumia tangu Juni mwaka huu,alimaliza jana wapili kutoka mwisho.Sasa anatarajia Holmes kuwa fit ili kushiriki katika mashindano yajayo ya jumuiya ya mandola-C-wealth games mjini Melbourne,Australia, mwezi machi mwakani.