Klopp: Kombe la Dunia la Vilabu ni wazo la "hovyo"
30 Juni 2025Matangazo
Klopp aliliambia gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag jana Jumapili kwamba kalenda ngumu haiwapi wachezaji nafasi ya kupumzika kimwili na kiakili, lakini pia uwezekano wa majeruhi.
Guardiola amesema anaielewa vizuri hoja ya Klopp, ambaye kwa pamoja waliipiga vita sana huko nyuma wakitaka wachezaji na makocha wapewe nafasi ya kupumzika ili kuimarisha viwango na ubora.
Hata hivyo licha ya kupingwa Guardiola amesema anatamani timu yake ichukue ubingwa wa michuano hiyo ya FIFA, akisema anajivunia kushindana na kushinda.