Ancelotti wa Real Madrid kuinoa timu ya taifa ya Brazil
29 Aprili 2025Matangazo
Hata hivyo, baada ya timu ya Real ya Ancelotti kuondolewa katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa na Arsenal na kushindwa na wapinzani wa jadi Barcelona kwenye michuano ya Kombe la Mfalme nchini Uhispania maarufu kama "Copa Del Rey", kunaashiria kuwa sasa muitaliano huyo yuko tayari kuondoka kabisa Santiago Bernabeu.
Vyombo vya habari vya Uhispania vimeripoti kuwa Ancelotti atachukua mikoba ya kuinoa timu ya taifa ya Brazil mnamo mwezi Juni, ambapo itakuwa ni kabla ya mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2026.