Kocha mpya Kovac apanga kuifufua Dortmund
10 Februari 2025Dortmund watacheza mechi ya kwanza ya mtoano katika Ligi ya Vilabu Bingwa kwenye Uwanja wa Sporting Lisbon Jumanne(11.02.2025), wakiwa wameshinda mechi tatu pekee kati ya 13 zilizopita.
Tayari walishatolewa nje ya mashindano ya Kombe la Ujerumani, Dortmund inashika nafasi ya 11 kwenye Bundesliga, pointi saba nje ya nafasi nne za juu na 25 nyuma ya viongozi wa ligi Bayern Munich kwa mechi 21 zilizochezwa.
Wakisaidiwa na sare ni wapinzani wawili pekee kati ya wanane wa Dortmund wa Ligi ya Mabingwa waliomaliza hatua ya makundi katika nusu ya kwanza ya jedwali wametulia katika nafasi ya 10 katika mchuano wa timu 36.
Dortmund watakabiliana na mabingwa wa Ureno Sporting, ambao wamekuwa na misukosuko yao kwenye kinyang'anyiro hicho tangu kuondoka kwa kocha Ruben Amorim kwenda Manchester United.
Soma pia: Ruben Amorim atangazwa kocha mpya wa Manchester United
Kocha wa zamani wa Bayern Munich, Eintracht Frankfurt na Monaco Niko Kovac alichukua nafasi ya Nuri Sahin ambaye alitimuliwa Januari, miezi saba tu baada ya kusaini kazi ndani ya Signal Iduna Park.
Hata hivyo Kovac ameanza kibarua chake kwa bahati mbaya. Baada ya kushindwa 2-1 nyumbani dhidi ya Stuttgart, Kovac alisema timu yake ilikuwa karibu na mabadiliko.
"Hatungekuwa na bahati mbaya zaidi. Timu ilijitolea kwa kila kitu. Kipigo kinaumiza kwa sababu kiliweza kuepukika," alisema.
Kuhusu mechi ya ugenini nchini Ureno, Kovac aliongeza "tunahitaji tu kufanya vitu kidogo hapa na pale, mabadiliko madogo.
"Vinginevyo tunahitaji kuwa waaminifu kwa yale ambayo tumeonyesha."
Kovac anajulikana kwa kuzingatia bidii na nidhamu, jambo ambalo alisisitiza katika ufunguzi wa mkutano wake na waandishi wa habari.
Hakuna haja ya madiliko makubwa
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 alisema hakuna haja ya mabadiliko ya jumla katika klabu hiyo na kwamba Dortmund ingerekebisha matokeo yake kwa kuzingatia vipengele vitano muhimu: "nidhamu, utaratibu, shauku, msukumo na ukali."
Vipengele hivi, vilivyowahi kuwepo katika ushindi dhidi ya Paris Saint-Germain, Atletico Madrid, Newcastle na AC Milan katika msimu uliopita wa kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa, vimekosekana sana msimu wa 2024-25.
Mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Sebastian Kehl, ambaye pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Sporting Lars Ricken walimleta Kovac kwenye klabu, wameunga mkono kauli ya kocha wao mpya.
Soma pia; Borussia Dortmund yaibwaga Celtic 7-1
Wakati kiwango cha Kovac mara nyingi kilimaanisha muda mfupi wa kufundisha -- hajawahi kufundisha zaidi ya michezo 100 katika klabu yoyote - mtindo wake unafaa zaidi kwa mashindano ya vikombe.
Alishinda Kombe la Ujerumani akiwa na Eintracht Frankfurt na kisha Bayern katika misimu mfululizo. Katika mwaka wake wa kwanza nchini Ufaransa, aliipeleka Monaco hadi fainali ya Kombe la Ufaransa, ambapo walipoteza kwa Paris Saint-Germain.
Katika msimu wake pekee kwenye Ligi ya Mabingwa, Bayern ya Kovac iliondolewa na Jurgen Klopp Liverpool msimu wa 2018-19.
Lisbon sio tishio
Kwa bahati nzuri kwa Kovac na Dortmund, Sporting hawana uwezekano wa kutoa changamoto kama hiyo.
Wakiwa bado kileleni mwa ligi ya Ureno, wametatizika tangu alipoondoka kocha Amorim na kutua Old Trafford. Chini ya Amorim, Sporting ilifungua dimba kwa kushinda mara tatu na kutoka sare moja, ikiwa ni pamoja na kuicharaza Manchester City mabao 4-1.
Tangu kuondoka kwa Amorim hata hivyo, Sporting wamepoteza mechi tatu na kutoka sare moja kati ya mechi zao za Ligi ya Mabingwa, wakishuka kutoka nafasi ya nane bora hadi 23.