JamiiAsia
Kisanduku cha mawasiliano ya ndege ya Air India chapatikana
13 Juni 2025Matangazo
Kisanduku hicho cha ndege, kilipatikana kwenye paa la nyumba karibu na eneo la ajali. Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, waziri wa usafiri wa anga Ram Mohan Naidu, amesema kupatikana kwa kisanduku hicho, kunaashiria hatua muhimu mbele katika uchunguzi .
Ajali ya ndege yaua zaidi ya watu 200 India
Kwa upande wake, Profesa Paul Fromme wa Taasisi ya Wahandisi wa Mitambo nchini Uingereza, amesema kwamba kisanduku hicho kina maelezo kuhusu injini na udhibiti wa mipangilio mbali na rekodi ya sauti katika chumba cha marubani.