KIRKUK:Mauaji ya kimadhehebu yazidi kasi Iraq
18 Septemba 2006Matangazo
Kiasi cha watu 23 wameuwawa na wengine wasiopungua 73 wamejeruhiwa katika wimbi la mashambulio ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari katika maeneo ya mji wa Kirkuk.
Katika shambulio baya zaidi mjini humo siku ya jumapili,mripuaji wa kujitoa muhanga aliendesha gari lililojazwa mabomu na kushambulia kituo cha polisi na ofisi mbili za vyama viwli vikuu vya kikurdi na kuua watu 17 wengi wakiwa ni raia.
Wakati huo huo mjini Baghdad polisi wamegundua maiti zaidi ya 24 za watu waliouwawa katika kile kinachoonekana kuwa ni mauaji ya kimadhehebu.