Kiongozi wa upinzani Uturuki amtembelea Meya aliye gerezani
25 Machi 2025Matangazo
Ozel, kiongozi wa Chama cha CHP cha Imamoglu, aliwasili katika gereza la Silivri, magharibi mwa Istanbul, akiandamana na msafara wa magari leo asubuhi.
Baada ya mkutano wa masaa mawili, Ozel aliwaambia waandishi wa habari kwamba anaona aibu kwa niaba ya wale wanaoiongoza Uturuki na kwa hali ilivyo nchini humo.
Jana usiku, Ozel alitangaza kuwa leo jioni, kutakuwa na mkutano wa hadhara wa mwisho nje ya ukumbi wa manispaa ya jiji la Istanbul, na akatoa wito kwa watu kushiriki, licha ya serikali kutangaza kupiga marufuku mikusanyiko.
Pia alisema chama hicho kitamteua mwanachama wa baraza la manispaa hiyo kukaimu wadhifa huo wa meya ulioachwa wazi na Imamoglu, ili kuzuia uwezekano wa serikali kumteuwa meya mpya.