SiasaRwanda
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda awekwa kizuizini
20 Juni 2025Matangazo
Idara ya kuchunguza uhalifu nchini Rwanda (RIB) imesema kuwa mwanasiasa mashuhuri wa upinzani, Bi Ingabire Victoire amekamatwa, kwa tuhuma za kuuchochea umma dhidi ya uongozi na kuunda kundi la wahalifu.
Victoire Ingabire alifikishwa mahakamani siku ya Alhamisi katika mji mkuu wa Kigali kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na kesi ya watu tisa wanaotuhumiwa kushiriki mafunzo yanayohusu jinsi ya kupindua serikali kwa kutumia njia zisizo za vurugu.
Ingabire ambaye anaongoza chama cha DALFA Umurinzi ambacho hakijasajiliwa, alirejea nchini Rwanda mwaka 2010 kutoka uhamishoni nchini Uholanzi, akiwa na nia ya kushindana na rais Paul Kagame katika uchaguzi wa rais, lakini alizuiliwa kwa tuhuma za kupinga kutokea kwa mauaji wa kimbari nchini Rwanda.