Kiongozi wa upinzani Israel ataka vita vya Gaza kukomeshwa
9 Juni 2025Golan, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Democrats na naibu mkuu wa zamani wa jeshi, ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache kabla ya kura iliyopangwa ya bunge ambayo upinzani unatumai itachochea uchaguzi mkuu. Amewaeleza waandishi wa habari kwamba baada ya mapigano ya zaidi ya miezi 20, yaliyochochewa na shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023, Israel "inapaswa kumaliza vita haraka iwezekanavyo". Chama cha Golan kina viti 4 pekee katika bunge la Israel lenye wanachama 120, na kukifanya kuwa moja ya makundi madogo zaidi ya kisiasa.Bunge la Israel lapitisha sheria tata ya mageuzi ya mahakama
Kiongozi huyo wa upinzani amesema kuwa idadi kubwa ya Waisraeli wanataka kuona vita ikimalizika mara moja huko Gaza, kurejea kwa mateka wote wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Kipalestina katika mpango mmoja wa mabadilishano na kuanzishwa kwa tume ya kitaifa ya uchunguzi kuhusu shambulio la Hamas mwaka 2023 ambalo halijawahi kushuhudiwa, akihoji kuwa serikali ya Netanyahu inapinga malengo hayo.
"Idadi kubwa ya watu wanataka uchaguzi mpya haraka iwezekanavyo, na idadi kubwa ya Waisraeli inataka kuifanya Israel kama nchi ya Wayahudi na wakati huo huo huru, usawa na serikali ya kidemokrasia."
Mwanasiasa huyo pia amesema kuwa Waisraeli wengi wanaunga mkono sheria ambayo itahitaji wanaume wa Kiyahudi wa dhehebu la Orthodox, ambao kwa sasa hawahusiki na utumishi wa kijeshi, kujiandikisha.Israel yasema itarejesha uingizwaji wa misaada Gaza
Suala hilo limezusha mvutano huku chama cha Kiorthodoksi cha Shas, kikitishia kuiangusha serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa kuunga mkono hoja ya uchaguzi wa mapema. Muungano wa Netanyahu, uko katika hatari ya kuporomoka kutokana na mswada ambao unaweza kutengua kinga ya muda mrefu kwa Wayahudi wa Kiorthodox kutotumikia jeshini.
Netanyahu anakabiliwa na shinikizo kutoka ndani ya chama chake cha Likud, kuwajumuisha wanaume zaidi wa Orthodox na kutoa adhabu kwa wale wanaokwepa muswada huo.
Kwenyewe Gaza, maafisa wa Palestina wameeleza kuwa vikosi vya Israel na washirika wake wamefyatua risasi dhidi ya umati wa watu uliokuwa ukielekea katika kituo cha ugawaji wa misaada kinachoungwa mkono na Israel na Marekani. Wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas imesema watu 6 wameuawa.
Wapalestina 25 wauawa wakati wakielekea kwenye kituo cha msaada Gaza
Mashahidi wameeleza kuwa maafisa waliofyatua risasi walionekana kuwa na mafungamnao na jeshi la Israel, wakitekeleza shughuli zao karibu na vikosi vya Israel sambamba na kurejea nyuma katika eneo la kijeshi la Israel katika mji wa kusini wa Rafah baada ya umati wa watu kuanza kuwarushia mawe.
Hili ni tukio la karibuni katika mkururo wa matukio ya ufyatuaji risasi ambayo yamewaua watu zaidi ya 127 na kujeruhi mamia wengine tangu kulipoanzishwa mfumo mpya wa ugawaji chakula, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas. Israel na Marekani zinasema mfumo huo mpya umebuniwa kuikwepa Hamas lakini umekataliwa na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine makubwa ya kiutu.