Kiongozi wa Syria, Ahmed Al sharaa atangaza serikali mpya
30 Machi 2025Serikali hiyo iliyo na mawaziri 22 ilitangazwa hapo jana katika sherehe rasmi iliyofanyika katika ikulu ya taifa mjini Damascus. Kuanzia Desemba hadi sasa Syria iliongozwa na serikali ya mpito iliyosimamiwa na waziri mkuu Mohammed al-Bashir, aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo kwa miezi mitatu baada ya kiongozi wa muda mrefu wa Syria Bashar al Assad kuondolewa madarakani mwezi uo huo.
Mawaziri wawili kutoka kwa serikali iliyopita Murhaf Abu Qasra na Asaad al-Shaibani, wameendelea kushikilia nafasi zao za ulinzi na masuala ya mambo ya nje.
Syria yatangaza kuunda Baraza la Usalama wa Kitaifa
Kulingana na duru kutoka Syria, serikali hiyo mpya haitokuwa na nafasi ya waziri mkuu na Al sharaa aliyeongoza mapambano ya kumuondoa Bashar Al Assad madarakani, anaesemekana kuwa uhamishoni nchini Urusi, atasimamia mwenyewe kazi ya Baraza lake la Mawaziri.