SiasaSyria
Kiongozi wa Qatar azuru Syria tangu kuangushwa kwa Assad
30 Januari 2025Matangazo
Taarifa ya ubalozi wa Syria nchini Sayria ilisema Sheikh Al-Thani anakwenda Damascus kwa mazungumzo ya kihistoria na rais wa mpito wa Syria, Ahmed al-Sharaa yatakayotuama juu ya ushirikiano na msaada kwa sekta kadhaa za maendeleo.
Tofauti na mataifa mengine ya kiarabu, Qatar haikusitisha mahusiano ya kidiplomasia na Syria wakati wa utawala wa Assad licha ya kuwa mojawapo ya nchi za mwanzo kuuunga mkono uasi uliozuka dhidi ya serikali ya Assad mwaka 2011.