KIONGOZI WA KWANZA KWENDA UTURUKI:
7 Januari 2004Matangazo
ANKARA: Rais Bashar el-Assad wa Syria amekutana na Rais Ahmet Necdet Sezer wa Uturuki mjini Ankara.Assad ni kiongozi wa kwanza wa Syria kuizuru Uturuki tangu Syria kujipatia uhuru wake mwaka 1946.Katika mkutano na waandishi habari Assad alisisitiza umuhimu wa kupata hali ya utulivu katika eneo lote la Mashariki ya Kati.Pia akatoa muito kuwa silaha za kinyuklia zipigwe marufuku katika eneo zima la Mashariki ya Kati ikiwa ni pamoja na Israel.Rais Assad akasema anakubaliana na msimamo wa Uturuki wa kupinga kuundwa Kurdistan huru kaskazini mwa Iraq.Rais Sezer kwa upande wake amesema uhasama na ukosefu wa utulivu ni mambo yanayopaswa kukomeshwa bila ya kupoteza wakati zaidi.Uhusiano kati ya Ankara na Damascus umekuwa na mivutano kwa miaka mingi kwa sababu ya mzozo wa mpakani kuhusika na matumizi ya maji kutoka mto Euphrates na pia madai kuwa Syria huwaunga mkono wanamgambo wa Kikurd walio nchini Uturuki.