Kim aamuru utayarifu wa silaha za nyuklia
28 Februari 2025Kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo (KCNA), jaribio hilo la silaha liliazimia kuwaonya wale lililowaita "maadui wanaoingilia mazingira ya kiusalama" ya nchi hiyo na kuonesha utayari wa njia zake mbalimbali za silaha za nyuklia.
Shirika hilo lilimnukuu Kim akisema ni jukumu la kikosi cha nyuklia kwenye jeshi la nchi yake kuwa tayari wakati wowote kuilinda Korea.
Soma zaidi: Kim akosoa ushirikiano kati ya Marekani, Korea Kusini na Japan
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka wizara ya ulinzi ya Korea Kusini, jeshi la Korea Kaskazini lilifanya majaribio yake ya makombora yanayosafiri kwa kasi baharini siku ya Jumatano.
Aina hiyo ya makombora haimo kwenye orodha ya yale yaliyopigwa marufuku na Umoja wa Mataifa, ingawa yanaweza kubeba vichwa vya nyuklia.