MigogoroSyria
Kiongozi wa kiroho wa Druze alaani mashambulizi dhidi yao
2 Mei 2025Matangazo
Hijri katika taarifa yake alilaani ghasia zilizotokea Jaramana na Sahnaya karibu na Damascus na kutoa wito kwa "jeshi la kimataifa" kuingilia mara moja ili kurejesha amani.
Katika hatua nyingine, Marekani imekutana na mwanadiplomasia mkuu wa Syria na kuzitaka mamlaka za nchi hiyo kuchukua hatua dhidi ya ghasia hizo zinazolenga jamii hiyo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Tammy Bruce amesema wawakilishi wa Marekani walikutana na ujumbe wa Syria mjini New York siku ya Jumanne na kuzitaka mamlaka "kuchagua sera zinazoimarisha utulivu."
Hayo yanafanyika, huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisema mapema leo kwamba wameshambulia kituo kilicho karibu na makazi ya rais mjini Damascus, kama sehemu ya kuwalinda watu hao.