Papa Leo XIV atoa wito wa amani duniani
11 Mei 2025Matangazo
Akizungumza katika viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican, mbele ya maelfu ya waumini waliojitokeza kwenye viwanja hivyo Papa Leo XIV ametoa wito wa amani ya kudumu Ukraine na kusitishwa kwa mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.
Soma zaidi: Papa Leo wa XIV ahimiza amani duniani katika sala yake ya kwanza ya baraka ya Jumapili
Ametaka pia mateka wa Israel wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas kwenye ukanda huo waachiliwe huru. Zaidi Papa Leo amesema amefurahi kusikia kuhusu makubaliano ya kusitisha vita kati ya India na Pakistan yaliyofikiwa Jumamosi na kuwa anamuomba Mungu aipe dunia muujiza wa amani.