Hezbollah imesema hawatasalimu amri kwa vitisho vya Israel
6 Julai 2025Matangazo
Qassem alisisitiza kuwa, "vitisho hivyo havitatufanya tukubali kusalimu amri.” Qassem, aliyemrithi Hassan Nasrallah aliyeuawa na Israel Septemba mwaka jana, amesisitiza kuwa Israel lazima ijiondoe kwenye maeneo ya Lebanon na kuachia wafungwa kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu usalama wa taifa.Tamko lake linakuja wakati mjumbe wa Marekani, Tom Barrack, anatarajiwa kuwasili Beirut kuwasilisha wito wa kuitaka Hezbollah ivunje nguvu zake za kijeshi kufikia mwisho wa mwaka huu. Hata hivyo, mashambulizi ya Israel yameendelea licha ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa Novemba.